Kundi la kwanza la zaidi ya Waislamu hao 1,600 kutoka Mnyanmar walisafirishwa hadi Bhasan Char mapema mwezi Disemba, na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje AK Abdulmomen amesema ni chini ya elfu moja walio katika kundi hili la pili.
Wakimbizi hao wanapelekwa katika kile anachokieleza ni kisiwa kizuri cha mapumziko.
Zaidi ya Warohingya 700,000 walikuwa wanaishi katika makambi nchini Bangladesh tangu 2017 baada ya mashambulio ya jeshi la Myanmar ambayo Umoja wa Mataifa wanasema huenda ni mauaji ya kimbari.
Baada ya kundi la kwanza kuhamishwa Disemba 4 baadhi ya Warohingya wameliambia shirika la Habari la AFP kwamba walipigwa na kulazimishwa kukubali kuhama.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa unasema haijahusishwa kwenye utaratibu huo.