Hichilema ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wakuu nchini humo, na pia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha UPND, ameyasema hayo mbele ya wanahabari wakati akiwa kwake nyumbani kwenye kitongoji cha Kanyama mjini Lusaka.
Hichilema ambaye amewania urais mara sita, Jumatatu alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais na kufikisha kikomo utawala wa miaka sita wa rais Edgar Lungu. Kiongozi huyo alipata jumla ya kura milioni 2.8 dhidi ya milioni 1.8 alizopata Lungu ikiwa ni zaidi ya asilimia 50 iliyo hitajika ili kutangazwa mshindi.
Lungu alikubali matokeo hayo wakati akiapa kuhakikisha ubadilishanaji madaraka wenye amani. Hata hivyo hapo awali muda mfupi baada ya uchaguzi kufanyika, Lungu alidai kuwa haukua wa haki na ukweli.