Seneti ya Marekani yashindwa kupitisha mswada wa kufadhili shughuli za serikali

Kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la Seneti ya Marekani, Chuck Schumer, akizungumza na waandishi wa habari.

Baraza la Seneti la Marekani Jumatatu lilishindwa kupitisha mswada wa kuzuia kufungwa kwa baadhi ya shughuli za serikali, ukiwa ni mwanzo mwa wiki yenye shughuli nyingi, ambazo zinadhihirisha changamoto zinazokabili bunge lenye mgawanyiko mkubwa.

Maseneta Warepublican walipiga kura kupinga mswada huo Jumatatu jioni, na kuwalazimisha Wademokrat kuanza kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha kwamba serikali itaendelea na shughuli zake baada ya Alhamisi wiki hii, na kuongeza viwango vya deni, kabla ya wakati ambapo inatarajiwa kushindwa kulipa madeni yake, mwishoni mwa mwezi Oktoba au mwanzoni mwa mwezi Novemba kufika

Maseneta 48 waliunga mkono mswada huo huku 50 wakipinga.

Angalau maseneta 60 wanahitajika kupitisha miswada mingi, kwa mujibu wa kanuni za baraza hilo.

Warepublican wamesema wanataka Wademokrat waongeze viwango vya deni peke yao kwa sababu wanaupinga mpango wao wa matumizi ya trilioni za dola.