Seneta Mstaafu wa Marekani Mike Enzi afariki dunia

Senata mstaafu wa Wyoming Mike Enzi alipokuwa akiwaaga wenzake desemva 2, 2020, mjini Washington Dc akiwaasa kulenga zaidi katika yale wanayokubaliana na sio sana katika wanayopingana.

Seneta Mstaafu wa Marekani Mike Enzi, Mrepublican wa Wyoming anayejulikana kama aliyekuwa mstari wa mbele kufikia muafaka katika Washington inayozidi kubadilika amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 77.

Enzi alifariki Jumatatu akiwa amezungukwa na wanafamilia na marafiki, msemaji wake wa zamani Max D'Onofrio alisema.

Enzi alikuwa amelazwa hospitali kutokana na kuvunjika shingo na mbavu baada ya kupata ajali ya baiskeli karibu na Gillette Ijumaa. Alikuwa na hali thabiti kabla ya kusafirishwa kwenda hospitali huko Colorado lakini alibaki amepoteza fahamu, D'Onofrio alisema.