Saudi Arabia yalaumiwa kwa kushambulia raia Yemen

Wanafunzi wakiwa katika jengo la shule lililo shambuliwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.

Watu 26 wameuwawa katika shambulizi la ndege kaskazini magharibu mwa Yemen, na mashirika ya haki za binadamu yameshutumu vikosi vya muungano unao ongozwa na Saudi Arabia kwa shambulizi hilo.

Mashambulizi ya Jumatano yalihusisha hoteli moja na soko la karibu katika jimbo la Saada. Jimbo hilo ambalo liko karibu na mpaka unaotenganisha Yemen na Saudi Arabia.

Vyanzo vya habari nchini Yemeni vimesema kuwa mashambulizi hayo yameendelea kuhusisha maeneo ya raia toka ilipoanzisha oparesheni zake katika kuiunga mkono serekali inayotambulika kimataifa ya Yemen Machi 2015.

Mgogoro huo umeshapoteza maisha ya watu 10,000 na kuzua mgogoro wa kibinadamu ambapo watu wamelazimika kukimbia makazi yao.

Waasi wa kihodhi, ambao waliuteka mji mkuu wa Yemen miaka mitatu iliyopita, wanalaumu muungano unaoongozwa na Saudi Arabia kwa kufanya mashambulizi hayo kwa raia.

Afisa wa mmoja wa afya nchini Yemen amethibitisha shambulizi hilo.