Uteuzi wa Jumatatu wa Sama Lukonde mshirika wa Rais Tshisekedi ni faraja kwa serikali yake ambapo atafanikisha kupata baraza la mawaziri wanaomtii na hivyo kushinikiza na kupitisha ajenda zake kiurahisi
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo-DRC Felix Tshisekedi amemteuwa Sama Lukonde kuwa Waziri Mkuu mpya nchini humo anazipa nafasi iliyoachwa na Sylvestte Ilunga Ilunkamba ambaye alijiuzulu zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Uteuzi huo umefurahiwa na pia umepokelewa kwa maoni mseto na wa Congo huku wengine wakielezea matumaini makubwa kuona vijana sasa wanapata fursa ya kushika nafasi za juu serikalini tofauti na hapo awali.
Mwandishi wa VOA Austere Malivika anaripoti kamili kutoka Goma.
Your browser doesn’t support HTML5