Rwanda yasema inao uhuru wa kujieleza

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Waziri wa sheria Jonhston Busingye amesema ni jambo la kushangaza kuendelea kuwepo kwa maoni hayo bila kutambua kuwa hilo limekuwa historia.

Serikali ya Rwanda imesema wale wanaoishutumu kwa kutoweka mazingira ya kutoa maoni au uhuru wa kujieleza ni wale wasiofahamu hali ilivyo na uhuru ulioko wa kutoa maoni.

Waziri wa sheria Jonhston Busingye amesema ni jambo la kushangaza kuendelea kuwepo kwa maoni hayo bila kutambua kuwa hilo limekuwa historia.

Your browser doesn’t support HTML5

Rwanda yasema inao uhuru wa kujieleza

Rwanda imekuwa ikisifika kwa kasi yake ya ukuaji wa kiuchumi, huduma nzuri kwa raia, usalama, ukomeshaji wa ulaji rushwa, lakini swala la kunyimwa uhuru wa kujieleza, na kutokuwepo mazingira bora ya kisiasa limeendelea kutoheshimiwa nchini humo.

Waziri huyo ameyasema hayo siku chache baada ya kurejea kutoka Geneva kwenye makao makuu ya tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu ambako Rwanda ilisikilizwa pamoja na mataifa mengine kuhusu yanavyotekeleza haki za binadamu.

Bw Busigye pia amesema Rwanda imekataa ombi kutoka tume hiyo la kutia saini mkataba wa kukubali mahakama ya kitaifa ya ICC. Rwanda imekuwa mstari wa mbele kulaumu mahakama hiyo kwa kuonea viongozi kutoka Afrika.