Rwanda inaadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyopelekea mauaji ya watu 800,000 katika mda wa siku 100.
Maadhimisho ya kitaifa yanafanyika katika mji mkuu wa Kigali.
Maadhimisho hayo yanafanyika bila kuwashirikisha watu wengi kutokana na janga la virusi vya Corona.
Katika miaka iliyopita, maadhimisho yalikuwa yakichukua wiki nzima.
Mauaji hayo yalitokea kufuatia kuaawa kwa aliyekuwa rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana, mhutu, ndege yake ilipopigwa risasi na kuanguka katika uwanja wa ndege wa Kigali, April 6 mwaka 1994.