Akiongea wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hali ya Mahakama mjini Nairobi Alhamisi, Dr Ruto amesema matumizi ya shilingi 7 bilioni tu ndio yanayo dadisiwa.
“Huenda ukawa umesikia kuwa serikali imepoteza kiasi cha Shilingi 21 bilioni huko Kimwarer na Arror ya mradi wa bwawa la maji, ambao ni uongo mtupu!” amesema akiwa Mahakama ya Juu.
“Pesa zinazodadisiwa ni kiasi cha shilingi 7 bilioni na kwa kila shilingi iliyolipwa, tunadhamana ya benki. Hakuna fedha itakayo potea kwa sababu sisi ni serikali yenye kuwajibika.”
Hata hivyo Makamu wa Rais Kenyatta hakutoa maelezo zaidi juu ya matumizi ambayo hayajatolewa ufafanuzi na juu ya madai ya kuwepo dhamana ya benki.
Makamu huyo ameutaka umma kujizuia kutoa madai ya ufisadi yasiyokuwa na uthibitisho, akisema kuwa hakuna fedha yoyote iliyopotea.
“Sio sawa kudai kuwa shilingi 9 bilioni zimepotea wakati mtu anafunguliwa mashtaka mahakamani kwa tuhuma za upotevu ea shilingo 100 milioni. Na hivyo Wakenya watauliza wakati huo zikowapi fedha nyingine shilingi 8.9 bilioni. Na tuwe wakweli,” amesema.
Majibu yake yamekuja siku moja baada ya kashfa kujitokeza inayohusu kampuni inayoshirikiana na Mkuu wa Wafanyakazi Ikulu, Ken Osinde, na vigogo wengine kadhaa pia wanakabiliwa na kashfa hiyo.
Osinde, balozi wa zamani nchini Ujerumani, Romania na Bulgaria, ameorodheshwa kama mkurugenzi wa kampuni ya Sanlam General Insurance Ltd, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Telkom Kenya na mkurugenzi mkuu wa zamani wa Kenya Vision 2030 delivery Board Mugo Kibati na ardhi iliyokuwa inamilikiwa na waziri John Michuki.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.