Ruto rais mteule Kenya

William Ruto Rais mteule wa Kenya.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amemtangaza Naibu Rais William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya, akiwa amepata zaidi ya asilimia 50.49 ya kura na kiongozi mkuu wa upinzani  Raila Odinga alishika nafasi ya pili akiwa amepata asilimia takriban 48.85 ya kura

Mgombea urais ili kutangazwa mshindi ni lazima apata asilimia 50 na kura moja. Wgombea wengine wawili ambao hawakupata hata asilimia moja ya kura ni George Wajackoyah na David Mwaure.

Mgombea urais Odinga hakufika Bomas kwenye eneo ambalo ni kituo rasmi cha IEBC ambacho kilikuwa kinakusanya matokeo ya kutoka katika kile kituo cha kupigia kura nchini humo.

Wakati huo huo Makamishna wanne wa IEBC awali walifanya kikao cha kushtukiza na wanahabari katika hoteli ya Serena, jijini Nairobi, ambapo wamesema hawakubaliani na matokeo yatakayotangazwa na mwenyekiti Wafula Chebukati.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation makamishna hao akiwemo makamu mwenyekiti Juliana Cherera, makamishna Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang'aya wamedai kuwa matokeo yalifikiwa kwa njia isiyoeleweka, bila kutoa maelezo zaidi.