Rais wa Kenya William Ruto amesaini kuwa sheria mswaada wa kwanza wa fedha wa serikali yake, unaolenga kuongeza mapato kwa kutoza kodi katika bidhaa kadhaa.
Moja ya mabadiliko yenye utata yaliyopitishwa na bunge wiki iliyopita ni kuongeza mara mbili zaidi ushuru wa ongezeko la thamani utakaotozwa kwenye mafuta kwa asilimia 16 kutoka asilimia 8.
Wafanyakazi wa serikali pia watatoa asilimia 1.5 ya mishahara yao kwa ajili ya malipo ya nyumba ambayo yatakwenda kwenye mpango ambao utalipia kujenga nyumba kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini.
Rais Ruto aliyechaguliwa mwaka jana alisema kwamba serikali inahitaji fedha zaidi ili iweze kulipia madeni yaliyokuwepo wakati wa mrithi wake Uhuru Kenyatta.
Lakini upinzani umesema utaitisha maandamano kama suala la tozo ya kodi litaanza kutekelezwa.