Kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC), imeamua kutowapiga marufuku wanariadha wote wa Russia kushiriki katika michezo ya mwaka huu mjini Rio De Jeneiro, kufuatia tuhuma za utumiaji uliokithiri wa dawa za kusisimua misuli. Akizungumza hii leo, mwenyekiti wa IOC, Thomas Bach, alisema kuwa kamati hiyo nusra iwapige marufujku wanariadha wote wa Russia waliotumia dawa hizo ili kulinda haki za wale ambao hawajazitumia dawa, na hivyo basi kuwapa fursa ya kushindana katika jukwaa la kimataifa.
Bach alisema kuwa ingawa ni rahisi kusema kuwa wanariadha wote wamepigwa marufuku kushirika kwenye mashindano hayo, ni vigumu kukutana nao ana kwa ana na kuwaelezea kuhusu uamuzi huo.
Hata hivyo, IOC, imesisitisha kuwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli vya wanariadha wa Russia vitafuatiliwa kwa makini kabisa wakati wa michezo yote ishirini na nane amabyo inatarajiwa kuanza tarehe tano mwezi ujao mjini Rio De Jenairo, Brazil.