Jenerali Oleksandr Syrskyi, kamanda wa vikosi vya ardhini vya Ukraine, amesema kwamba wanajeshi wa Russia wamezidisha mashambulizi ya makombora kwa kutumia silaha nzito dhidi ya mji huo, na wameanza kutumia vifaa vya kisasa na kupanga upya wanajeshi.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha ripoti hizo.
“Leo, ni muhimu sana kuchukua maamuzi haraka iwezekanavyo ili kuzuia vitendo vya adui,” Syrskyi alisema kwenye mtandao wake wa Telegram baada ya kile alichosema ilikuwa kuwajulia hali wanajeshi ambao wako kwenye mapambano katika mji wa Bakhmut.
“Russia bado wanatumai kuuteka mji huo ifikapo tarehe 9 Mei. Wajibu wetu ni kuzuia hilo lisitokee.”
Tarehe 9 Mei ni maadhimisho ya siku ya ushindi nchini Russia ikiwa kumbukumbu ya ushindi dhidi ya utawala wa Wanazi wa Ujerumani.