Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema ukweli huo ni kuhusu maeneo manne ya Ukraine ambayo ilitangaza mwezi Septemba kuwa maeneo huru chini ya udhibiti wa Russia, hatua ambayo Umoja wa Mataifa ulilaani kuwa si halali.
Peskov alikuwa akijibu kuhusu ombi la rais Zelenskiy kwa viongozi wa kundi la G7 jana Jumatatu kupewa vifaa zaidi vya kijeshi, msaada wa kifedha na uthabiti wa nishati, na kuunga mkono suluhisho la amani ambalo litaanza kwa Russia kuondoa wanajeshi wake nchini Ukraine, kuanzia Krismasi hii.
Peskov amesema “Kuna hatua tatu kuelekea kumaliza uhasama”, akiongeza kuwa Ukraine inahitaji kuzingatia hali halisi inayoendelea wakati huu.
Amesema “Ukweli huu unaonyesha kuwa maeneo mapya yamepatikana ndani ya shirikisho la Russia, na yalipatikana kama matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika katika maeneo hayo.”
Hilo likizingatiwa, hakuna budi kwa Russia kuanza kuondoa