Russia yatishia vita zaidi iwapo meli za kivita zitasindikiza meli za mizigo kutoka Ukraine

Meli za vita za Russia katika Black sea. Apr. 22, 2021

Russia imesema kwamba ipo tayari kuruhusu meli zilizobeba chakula kuondoka Ukraie iwapo tu baadhi ya vikwazo ilivyowekewa vitaondolewa.

Haya ni kulingana na shirika la habari la Interfex, ambalo limemnukuu naibu wa Waziri mkuu wa Russia Andrei Rudenko.

Bandari za Ukraine zilizo black sea zimefungwa tangu Russia ilipoanza kuvamia Ukraine Februari 24 na zaidi ya tani milioni 20 za nafaka zimekwamba katika magala ya Ukraine.

Russia na Ukraine huzalisha theluthi tatu ya ngano inyotumiwa kote duniani na ukosefu wa usafirishaji wa bidhaa hiyo imechangia ukosefu wa ngano katika masoko ya kimataifa.

Ukraine pia ni mzalishaji mkubwa wa mahindi na mafuta ya kupika.

Nchi zenye nguvu duniani zimekuwa zikijadiliana namna ya kuwezesha nafaka na ngano kusafirishwa kutoka Ukraine kwa njia salama.

Russia na Ukraine zimeshutumiana kwa kutega mabomu baharini kuzuia usafiri wa meli.

Naibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Russia Rudeko, amesema kwamba iwapo meli za Ukraine zitasindikizwa na meli za kivita za mataifa ya magharibi, mgogoro utaongezeka zaidi.