Russia yapoteza wanajeshi 376,030 tangu kuivamia Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa Saint Petersburg Julai 27, 2023. Picha na Valery SHARIFULIN / Wakala wa Picha Mwenyeji wa TASS / AFP.SSIA-AFRICA-DIPLOMACY

Russia imepoteza wanajeshi 376,030 tangu kuivamia Ukraine, jeshi la Ukraine lilisema Jumapili. Idadi hiyo pia inajumuisha majeruhi 760 siku moja kabla.

Russia pia imepoteza idadi kadhaa ya magari na vifaa katika mapambano hayo, kulingana na ripoti, ikiwa ni pamoja na magari ya kivita 11,466, magari 11,862 na matanki ya mafuta, na mizinga 6,181. Russia haijatoa maoni kuhusu idadi hiyo ya hivi karibuni.

Darzeni ya watu waliuwawa au kujeruhiwa Jumapili katika shambulizi la makombora kwenye soko nje kidogo ya mji wa Donetsk katika eneo la Ukraine linalokaliwa kimabavu na Russia.

Alexei Kulemzin, meya wa Tekstilshchik aliyewekwa na Russia, alisema shambulio hilo lilitoka Ukraine.