Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:31

Russia yadai kunasa na kuharibu silaha za Ukraine kwenye Peninsula ya Crimea


Wingu wa moshi ukupaa angani kufatia shambulizi la bomu kwenye daraja la Peninsula ya Crimea, July 19, 2023.
Wingu wa moshi ukupaa angani kufatia shambulizi la bomu kwenye daraja la Peninsula ya Crimea, July 19, 2023.

Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema kwamba vikosi vya ulinzi wa hewa vya Russia vimenasa na kuharibu silaha za Ukraine zilizorushwa kwenye anga ya Crimea Jumamosi.

Wizara hiyo imeongeza kusema kwamba vikosi hivyo pia vilidungua droni kadhaa zilizorushwa Ijumaa usiku kwenye Peninsula ya Crimea pamoja na sehemu ya magharibi ya bahari ya Black Sea. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy awali aliahidi kuongeza mashambulizi kwenye Peninsula ya Crimea na ndani ya Russia mwaka huu, suala ambalo limezua wasiwasi nchini humo wakati Vladimir Putin akiwania tena wadhifa wake kwenye uchaguzi wa Machi.

Kwenye mji wa Belgorod uliyopo kwenye mpaka wa kusini mwa Russia, maafisa wamekuwa wakijitahidi kuokoa wakazi wanaotafuta usalama kutokana na mashambulizi. Gavana wa mji huo Vyacheslav Gladkov kupitia ujumbe wa video wa Ijumaa amesema kwamba mafisa wake tayari wameokoa familia kadhaa.

Wakati huo huo, wizara ya Ulinzi ya Uingereza mapema leo kupitia kwenye ukurasa wake wa X imesema kwamba idadi ya vifo vya kila siku vya wanajeshi wa Russia ndani ya Ukraine viliongezeka hadi karibu 300 kufikia mwishoni mwa mwaka uliyopota.

Forum

XS
SM
MD
LG