“Tunaiangalia maendeleo ya hali ilivyo, lakini hadi hivi sasa tunashukuru Mungu kwa kuwa ipo kwenye ngazi za maneno tu,” Msemaji wa Kremlin Dmitry Psekov amewaambia wanahabari Alhamisi.
"Eneo la Arctic ni eneo letu kitaifa na maslahi ya kimkakati. Tuko katika eneo la Arctic, na tutaedelea kuwepo huko," Peskov alisema. Eneo kubwa la Greenland ambalo liko juu ya Mzunguko wa Arctic rasmi limekuwa sehemu ya himaya ya ufalme wa Denmark tangu 1953, ingawa kisiwa hicho kina serikali yake.
Wakati akizungumza na wanahabari Jumanne nyumbani kwake Florida, Donald Trump alisema kuwa Marekani inaitaka Greenland kwa malengo ya kiusalama na kukataa kufuta uwezekano wa kutumia njia za uchumi na kijeshi kufanikisha lengo hilo.
“Watu hata hawajui kama Denmark ina haki yoyote ya kisheria kufanya hivyo. Lakini kama wakifanya hivyo, waliachie kwasababu tunalihitaji kwasababu za usalama wa taifa," Trump alisema.