Wizara ya ulinzi ya Uingereza Ijumaa imesema katika taarifa yake ya kila siku ya kijasusi kuhusu uvamizi wa Russia, nchini Ukraine kwamba Russia, imewekeza katika uboreshaji mkubwa wa usalama wa kituo kikuu cha meli katika Black Sea huko Sevastopol toka 2022.
Yale yaliyo jumuishwa katika uwekezaji huo ni shughuli za mafunzo ya wanyama wa baharini kulingana na taarifa za sasa.
Wanyama hao huwenda wakawa ni Dolphin kwa muibu wa ripoti hiyo ambayo inasema kwamba wanatarajiwa kwa kiwango kikubwa kukabiliana na maadui wapiga mbizi.
Wizara hiyo imesema Russia, imefundisha wanyama kwa mipango kadhaa na katika bahari ya Arctic ambapo hutumiwa nyangumi na wanyama wengineo.
Wizara, hata hivyo, haikufichua ni oparesheni gani ambayo imefanya wanyama hao kupelekwa eneo la Arctic.