Russia yaendelea kukanusha kuhusika na shambulizi la hospitali Ukraine

Hospitali ya Watoto ya Okhmatdyt iliyoshambuliwa na Russia, mjini Kyiv, Ukraine, Julai 9, 2024.

Huku shambulizi la bomu katika hospitali ya watoto mjini Kyiv likilaumiwa kote ulimwenguni, maafisa wa Russia, wamekanusha nchi yao kuhusika na shambulizi hilo.

Maafisa hao pia wanajaribu wakijaribu kuelekeza lawama kwa Ukraine na washirika wake wa Magharibi.

Shambulizi la Julai 8 katika hospitali ya watoto ya Okhmatdyt, jijini Kyiv, limefanyika wakati kukiwa na msururu wa mashambulio kote Ukraine ambayo yashauwa watu 43, wakiwemo watoto.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amelaani vikali shambulio hilo la bomu na kusema kwamba Russia lazima iwajibike.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura Jumanne kuhusiana na mashambulizi hayo baada ya maombi kutoka kwa washirika wa Kyiv.