Russia yaanza mazoezi ya kijeshi ya baharini  na China na Iran

Rais wa Russsia Vladimir Putin akisalimiana na Mkuu wa Sera ya Kigeni wa Chama cha Kikomunisti cha China Wang Yi wakati wa mkutano wao kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Jumatano, Februari 22, 2023. AP

Russia ilisema Jumatano imeanza mazoezi ya kijeshi ya baharini  na China na Iran katika Bahari ya Arabia wakati ikijaribu kuimarisha uhusiano wake na Beijing na Tehran.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema katika taarifa yake kwamba mazoezi hayo ya pande tatu yaliyopewa jina la Marine Security Belt 2023 yameanza katika eneo la bandari ya Chabahar ya Iran.

Sehemu ya majini ya mazoezi hayo itafanyika Alhamisi na Ijumaa.

Russia itawakilishwa na meli ya kijeshi ya the Admiral Gorshkov frigate na meli ya ukubwa wa kati wizara hiyo ilisema.

Wakati wa mazoezi hayo ya wanamaji meli zitafanya mbinu za pamoja na zitarusha mizinga mchana na usiku ilisema taarifa hiyo.