Russia na Ukraine zimeshambuliana kwa ndege zisizokuwa na rubani

Kifaru cha Ukriane karibu na Pokrovsk, the eastern Donetsk. December 13, 2024. (Photo by Roman PILIPEY/AFP

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limeangusha ndege zisizokuwa na rubani 36 kati ya 60 zilizorushwa na wanajeshi wa Russia dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia leo.

Jeshi la anga la Ukraine limesema mashambulizi ya Russia yametekelezwa katika miji ya Chernihiv, Dnipropetrovsk, Kharkiv, Khmelnytskyi, Kyiv, Poltava, Sumy na Zaporizhzhia.

Nyumba kadhaa zimeharibiwa, sawa na mfumo wa umeme.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kwamba mfumo wake wa ulinzni umeharibu ndege nne zisizokuwa na rubani zilizorushwa na Ukraine, ikiwemo katika mkoa wa Rostov na katika sehemu za Voronezh, kwenye mpaka wa Russia na Ukraine.

Magavana wa mikoa ya Rostov na Voronezh, wameandika ujumbe wa Telegram kwamba hakuna uharibifu umeripotiwa kutokana na mashambulizi ya Ukraine.