Russia na Ukraine zashambuliana kwa ndege zisizo na rubani

Waokoaji wakimuondoa muathirika wa kombora la Russia katika mji wa Kharkiv, Ukraine Septemba 1, 2024. Picha na REUTERS/Yevhen Titov

Russia na Ukraine kila moja ilifanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani siku ya Jumatano, huku afisa wa Marekani akithibitisha kuwa hivi karibuni Marekani itawapatia mabomu  ya ardhini ili yatumiwe na  vikosi vya Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema ilizitungua takriban ndege 50 za Ukraine zisizo na rubani, huku uzuiaji ukiendelea katika mikoa ya Novgorad, Kursk, Oryol, Belgorod, Tula, Tver, Bryansk, Moscow na Smolensk.

Jeshi la anga la Ukraine limesema Russia ilishambulia kwa ndege 122 zisizo na rubani, huku makombora ya ulinzi ya anga ya Ukraine yakiangusha 56 kati yao. Mashambulizi hayo ya angani yalilenga mikoa ya Cherkasy, Chernihiv, Dnipropetrovsk, Donetsk, Kharkiv, Khmelnytksyi, Kirovohrad, Kyiv, Mykolaiv, Poltava, Sumy, Zaporizhzhia na Zhytomyr ya Ukraine.