Russia na China zimemaliza mazoezi ya kijeshi katika bahari ya Japan

Meli za kivita za Russia na China katika mazoezi

China na Russia zimemaliza mazoezi ya pamoja na kijeshi katika bahari ya Japan, ambayo wamesema yanalenga kuimarisha usalama wa usafirishaji wa bidhaa baharini.

Wizara ya ulinzi ya China imesema kwamba mazoezi hayo yamefanyika ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kulinda usalama wa utulivu katika kanda hiyo.

Mazoezi hayo yalihusisha kusindikiza meli na ndege, kuzuia kushambuliwa pamoja na ulinzi wa jumla.

Russia imesema kwamba zaidi ya ndege za kijeshi 30 zilihusika katika mazoezi hayo, ikiwemo manowari za ulinzi, ndege za helikopta na mifumo ya kunasa makombora.