Mazoezi hayo ya kijeshi yaliyopewa jina la “Ocean 24,” yanahusisha wanajeshi wa China na yatafanyika hadi tarehe 16 Septemba, na takriban nchi 15 zimealikwa kufuatilia mazoezi hayo, kulingana na wizara ya ulinzi ya Russia.
Rais wa Russia Vladimir Putin alisema Russia “inakuwa makini sana” katika kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na “nchi rafiki” na aliionya Marekani kutojaribu kuiondoa Moscow huko Asia.
Wachambuzi wanasema mazoezi hayo ya pamoja ni juhudi za Russia na China kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kukabiliana na ushirikiano mkubwa wa pamoja wa kiusalama kati ya Marekani na washirika wake katika kanda ya Indo-Pacific.