Russia kuzuia azimio la G20

Russia itazuia azimio la mwisho la mkutano wa mwezi huu wa G20 labda tu liweke wazi nafasi ya Moscow kuhusiana na Ukraine na migogoro mingine, na kuwafanya washiriki kutoa taarifa isiyo fungamana ama ya pamoja amesema waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov, Ijumaa.

Lavrov ambaye amehudumu kama waziri wa mambo ya nje chini ya rais Vladimir Putin toka mwaka 2004, anatarajiwa kuiwakilisha Russia katika mkutano wa kundi la nchi 20 zilizo endelea kiviwanda na zinazo endelea wa Septemba 9 na 10 mjini New Delhi.

Rais Putin haijajulikana kama amewahi kusafiri nje ya nchi toka mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutoka hati ya kukamatwa kwake mwezi Machi kwa kuhusishwa kwa vitendo vya uhalifu wa kivita.

Kremlin inavielezea vita vya Ukraine ambavyo vimeanza baada ya Russia kufanya uvamizi Febuari 2022, kama mapambano dhidi ya kiburi cha mataifa ya Magharibi.