Urais wa Russia katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ni pigo kwa jumuiya ya kimataifa, amesema waziri wa mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba kupitia ujumbe wa Twitter.
Russia ilichukua uongozi wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Jumamosi ambao huzunguka kila mwezi.
Mara ya mwisho Moscow kushika wadhifa huo ilikuwa Februari 2022, wakati wanajeshi wake walipoanzisha uvamizi kamili wa Ukraine.
Hayo yanatokea wakati Marekani ikitarajiwa kuongeza misaada mipya ya kijeshi kwa Ukraine yenye thamani ya dola bilioni 2.6 ambayo inaweza kujumuisha rada za uchunguzi wa anga, roketi za kukinga vifaru na malori ya mafuta kwa Ukraine wamesema maafisa wa Marekani.
Jumamosi wizara ya ulinzi ya Russia kupitia Telegram ilitoa video ya waziri wa ulinzi wa Russia, Sergei Shoigu akiahidi kuongeza usambazaji wa silaha kwa vikosi vya Russia vilivyopo Ukraine.