Russia kutoa maelezo ya kina kwa Afrika kuhusu usafirishaji wa chakula kutoka Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin

Ukraine ni mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa ngano, mahindi na mafuya ya kupika.

Maafisa wa Ukraine na mataifa ya magharibi, yameishutumu Russia kwa kuzia usafirishaji wa chakula kutoka bandari za Ukraine.

Russia imekanusha ripoti za kuzuia usafirishaji wa chakula kutoka Ukraine, na badala yake imesema kwamba Ukraine inastahili kuondoa mabomu yaliyotegwa baharini ili kuziwezesha meli kupita.

Msemaji wa Russia Dmitry Peskov, amesema kwamba Putina anapanga kutoa maelezo ya kina kwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika Macky Sall, kuhusu mtazamo wa Russia namna hali ilivyo nchini Ukraine na kinachostahili kufanyika ili kuruhusu nafaka kusafirishwa.

Kulingana na umoja wa mataifa, nchi za Afrika ziliagiza asilimia 44 ya ngano kutoka Ukraine na Russia kati ya mwaka 2018 na 2020.