Russia imeshambulia Ukraine kwa ndege zisizokuwa na rubani

Uharibifu uliofanywa na ndege zisizokuwa na rubani za Russia, Odesa Nov 9 2024

Ndege za Russia zisizokuwa na rubani, zimeshambulia bandari ya Odesa katika black sea usiku wa kuamkia leo na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine 13, wakiwemo wavulana wawili.

Hayo ni kulingana na gavana wa mkoa huo Oleh Kiper.

Nyumba kadhaa za makaazi ya watu, nyumba binafsi, majengo ya biashara na darzeni ya magari binafsi vimeharibiwa katika mashambulizi ya mfululizo ya ndege zisizokuwa na rubani katika mji huo.

Wavulana waliouawa wana umri kati ya miaka minne na 16.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba Russia ilianzisha msururu wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Odea na sehemu za karibu kusini mwa Ukraine, na kuongezea kwamba mfumo wa ulinzi wa Ukraine ulinasa na kuharibu ndege zisizokuwa na rubani za Russia 32.