Msemaji wa wizara ya nje ya Russia Maria Zakharova, amesema kwamba hatua ya Marekani kupeleka makombora ya kujilinda kunasa makombora ya Russia ni hatua ya Marekani kujiingiza zaidi katika mgogoro huo na ya kusaidia Ukraine katika vita hivyo ambavyo zimeingia mwezi wa kumi.
Russia imeonya kwamba hatua hiyo itakuwa na athari zake.
Zakharova hajasema hatua zitakazochukuliwa na Moscow, lakini amesema kwamba Marekani inastahili kuthathmini hatua yake kutokana na onyo la Russia kwamba silaha zinazotolewa na Marekani kwa Ukraine zinalenga mashambulizi yanayotekelezwa na Russia.
Amesema kwamba Marekani sasa imekuwa sehemu ya moja kwa moja katika vita hivyo.
Tayari Marekani imetoa mafunzo kwa karibu wanajeshi 3,100 wa Ukraine, namna ya kutumia silaha hizo.