Russia imefanya mashambulizi ya Drone nchini Ukraine

Mfano wa Drone zinazotumika na Russia katika mashambulizi yake kwa Ukraine

Kituo kikuu cha gridi ya taifa Ukrenergo kilisema kituo cha nishati katika mkoa wa Sumy kiliharibiwa

Russia imefanya shambulizi la ndege zisizokuwa na rubani-Drone usiku wa kuamkia leo nchini Ukraine, limepiga kituo cha nishati katika mkoa wa Sumy ulioko kaskazini mashariki mwa nchi, maafisa walisema.

Makundi ya Drone na vitengo vya ulinzi wa anga vya Ukraine vilitungua ndege 24 kati ya 27 za Russia zilizorushwa katika mikoa 12, kitengo cha anga kilisema.

Kituo kikuu cha gridi ya taifa Ukrenergo kilisema kituo cha nishati katika mkoa wa Sumy kiliharibiwa, na kulazimisha umeme wa dharura kuzimika kwa watumiaji wa viwanda katika mji wa Sumy.

Timu za kufanya matengenezo zilikuwa zikifanya kazi ya kurejesha huduma, ilisema taarifa. Hakuna taarifa za haraka za vifo au taarifa za kina za uharibifu mwingine kutoka kwenye mikoa.