Rais wa zamani wa Iran, Hassan Rouhani, Jumatano ametangaza kumuunga mkono mgombea mpenda mageuzi Masoud Pezeshkian, siku mbili kabla ya uchaguzi ambao haukutarajiwa kuchukua nafasi ya marehemu Rais Ebrahim Raisi.
Rouhani, mwanasiasa mwenye msimamo wa wastani mtangulizi wa Raisi, amesema Pezeshkian, ni mwanamageuzi pekee kati ya wagombea anayeweza kuondoa kivuli cha vikwazo ambavyo vimeathiri uchumi wa Irani toka kuanguka kwa makubaliano ya kihistoria ya nyuklia.
“Siku ya Ijumaa, tunapaswa kumpigia kura mtu ambaye amedhamiria kuondoa kivuli cha vikwazo kutoka kwa watu wa Irani,” Rouhani amesema katika ujumbe wa video uliwekwa na mtandao wa kimageuzi wa Shargh Daily, akisifu uaminifu wa Pezeshkian.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa rais Raisi katika ajali ya helikopta mwezi uliopita.