Ripoti ya uchunguzi wa ghasia Afrika kusini yagundua kushindwa kwa mfumo wa ujasusi

Baadhi ya majengo yalionekana kuwaka moto kufuatia ghasia za Afrika kusini. Durban, July 14, 2021.

Vikosi vya usalama vilielemewa na ghasia za Julai mwaka 2021 ripoti iligundua katika machafuko ambayo yalikuwa mabaya zaidi katika enzi ya demokrasia ya Afrika kusini

Ghasia mbaya zilizoikumba Afrika kusini baada ya Rais wa zamani nchini humo Jacob Zuma kufungwa mwaka 2021 zilifichua mapungufu makubwa ya kijasusi yaliyofanywa na polisi kulingana na uchunguzi uliotolewa Jumatatu.

Vikosi vya usalama vilielemewa na ghasia za Julai mwaka 2021 ripoti iligundua katika machafuko ambayo yalikuwa mabaya zaidi katika enzi ya demokrasia ya Afrika kusini. Ripoti hiyo ni matokeo ya uchunguzi wa jopo lililoteuliwa na serikali jinsi ghasia hizo zilivyoshughulikiwa na iliwekwa wazi na Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa hii leo.

Kulikuwa na kushindwa kwa mfumo wa kijasusi kushiriki na kujibu ipasavyo vurugu hizo iligundua ripoti hiyo. Ripoti ilisema huduma za kijasusi zilishindwa kutabiri hali ya mazingira, kiwango, na njia ya uendeshaji ya vurugu. Wakati huo huo polisi walikuwa na uwezo wa kutosha wa kuzuia ghasia hizo.