Ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama cha Republican ulichukua muda wa dakika kumi tu Jumatatu mchana na kuahirishwa hadi Jumanne asubuhi ambapo shughuli rasmi zitaanza kuelekea uteuzi wa Gavana wa zamani wa Massachussetts, Mitt Romney, kama mgombea urais wa chama cha Republican.
Saa nane mchana Jumatatu maafisa wa ngazi za juu wa chama cha Republican wataingia katika ukumbi wa mkutano na kutangaza rasmi kufunguliwa kwa mkutano na hapo hapo kuuahirisha hadi jumanne asubuhi. Shughuli hiyo itachukua muda wa dakika kumi tu.
Uamuzi wa kuahirisha kuanza rasmi kwa shughuli za mkutano jumatatu ulichukuliwa siku mbili zilizopita kutokana na utabiri wa hali ya hewa kwamba kimbunga Isaac kilikuwa kinaelekea katika mji huu uliopo magharibi mwa jimbo la Florida.
Hata hivyo kimbunga Isaac kinaelekea kutoathiri eneo la mji wa Tampa na badala yake kuelekea maeneo mengine ya ghuba. Kwa hiyo matazamio yote yameelekezwa kesho jumanne.
Maelfu ya wajumbe wa mkutano huu kutoka majimbo yote ya marekani wamekwishaingia Tampa wakati chama cha Republican kinajiandaa kumteua rasmi Mitt Romney.
Chama cha Republican kinatazamia kutumia fursa hii kumtambulisha Romney kwa wamarekani kama mtu anayeelewa hisia za wamarekani wa kawaida. Hilo limekuwa tatizo kubwa kwa Romney akilinganishwa na Rais Barack Obama ambaye – bila kuzingatia sera wamarekani wanaelekea kumpenda tu.
Romney ambaye ni mtu tajiri nchini humu amekuwa akipata shida kuwaonyesha wamarekani kwamba anajua matatizo yote, na viongozi wa chama cha Republican wanatumaini katika mkutano huu kulainisha hiba ya Romney katika macho ya wamarekani.
Miongoni mwa maswala muhimu yatakayofanyika jumanne katika siku ya kwanza ya mkutano ni wajumbe wa mkutano kuidhinisha maswala muhimu ambayo chama hiki kitawasilisha kwa wananchi wa Marekani katika juhudi zake za kuingia katika uongozi wa taifa.
Your browser doesn’t support HTML5