Mkutano wa chama cha Republican unamalizika Tampa

mgombania kiti cha rais wa chama cha Republican Mitt Romney,(kushoto) na mgombea mwenza wake l Paul Ryan Aug. 31, 2012

Matazamio ni makubwa sana leo kwani hii Imekuwa safari ndefu kwa mitt Romney kufika hapa – safari iliyochukua zaidi ya miaka minne na hatimaye leo gavana huyo wa zamani wa jimbo la Massachussets atapokea rasmi uteuzi wa chama cha Republikan kuwa mgombea wake urais katika uchaguzi mkuu mwezi novemba.

Wasikilizaji wetu watakumbuka kuwa Romney aliwania ugombea wa chama hicho mwaka 2008 lakini akashindwa na seneta John Mccain – na mwaka huu alipambana vikali na warepublican wengine tisa, na baada ya miezi kadha ya kampeni hatimaye mapema wiki hii kwa kura za wajumbe zaidi ya elfu mbili aliteuliwa rasmi kuwa mgombea wa chama hicho hapa katika mkutano wa uteuzi.

Your browser doesn’t support HTML5

Mkutano mkuu wa Republican unamalizika Tampa


Mitt Romney alikubali rasmi kuwa mgombea siku ya Alhamisi na kukamilisha tiketi ya chama cha Republikan – akiwa na mgombea mwenza Paul Ryan – kupambana na rais Barack Obama katika uchaguzi mkuu Novemba.

Kinachosubiriwa kwa hamu leo ni hotuba ya Romney, endapo itafanana na tukio ama la. Lakini wachambuzi wanasema Romney amepata mazoezi ya kutosha katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja uliopita ambapo amekuwa akitoa hotuba kadha kama hizi.

Kwa wiki nzima hii, hotuba za wazungumzaji wengine wakuu zilikuwa zinajenga hoja ya mitt Romney leo usiku. Jumatano usiku mgombea mwenza wake paul ryan alitoa hotuba ambayo ilipokelewa vizuri na wajumbe wa republican, ingawa wachambuzi wanasema ilikuwa na mengi ya kuulaumu utawala wa Obama kuliko sera za tiketi ya Romney na Rayn.

Mkutano mkuu wa chama cha Republican wamalizika Tampa


Ila Jumatano usiku waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice aliwakosha warepublican kwa hotuba yake ambayo ilikita zaidi katika sera za mambo ya nje na kuonyesha wazi wazi uzoefu wake katika maswala ya uhusiano wa Marekani na mataifa ya nje.

Bi Rice alikuwa mwanamke wa kwanza – Mmarekani mwenye asili ya kiafrika – kuhutubia kama mmoja wa wazungumzaji wakuu katika historia ya mkutano mkuu wa uteuzi wa chama cha Republikan