Rasoulof anaiomba jumuia ya filamu iwalinde watengeneza filamu wenzake

Mohammad Rasoulof, mkurugenzi wa filamu aliyekimbia nchini Iran.

Rasoulof alitoroka Iran baada ya kubainika amehukumiwa kifungo cha miaka minane kwa kuvujisha taarifa za usalama wa taifa.

Mkurugenzi wa filamu Mohammad Rasoulof ambaye kwa siri ameikimbia Iran kwenda eneo lisilojulikana barani Ulaya alitoa wito Jumanne kwa jumuiya ya filamu duniani kutoa msaada mkubwa kwa wenzake.

Rasoulof ambaye alihukumiwa kifungo kwa mashtaka ya usalama wa taifa, na ambaye filamu yake ya hivi karibuni itashindana katika tamasha la filamu la Cannes mwezi huu, alisema anahofia “usalama na ustawi” wa watengenezaji filamu wenzake, ambao bado wako nchini Iran.

Mtengenezaji filamu raia wa Iran, Mohammad Rasoulof.

“Jumuiya ya filamu ya kimataifa lazima itoe msaada mkubwa kwa watengenezaji wa filamu hizi”, Rasoulof alisema katika taarifa kwa shirika la habari la Agence France-Presse. Rasoulof alitangaza siku ya Jumatatu kuwa ametoroka kwa siri kutoka Iran, siku chache baada ya kubainika kuwa amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa “kuvujisha taarifa za usalama wa taifa.

Rasoulof alikuwa kwenye shinikizo kutoka kwa mamlaka ya Iran kuiondoa filamu yake ya hivi karibuni, “The Seed of the Holy Fig”, kutoka Cannes, ambapo itashindana kwenye tuzo ya juu kabisa inayotolewa na Cannes ya Palme d'Or.