Ramaphosa amechaguliwa kuongoza ANC, atashinda mawimbi ya kisiasa kufikia uchaguzi mkuu 2024?

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa baada ya kuhutubia kongamano la biashara mjini Cape Town, Afrika kusini. Dec 6, 2022

Cyril Ramaphosa, rais wa Afrika kusini, amechaguliwa wiki hii kuwa mwenyekiti wa chama kinachotawala cha African national Congress ANC.

Ramaphosa amechaguliwa kuendelea kuongoza ANC siku chache baada ya kunusurika kura ya kutokuwa na Imani naye bungeni.

Anaandamana na kashfa ya utakatishaji wa pesa. Ripoti ya kwanza kutaka achunguzwe zaidi imezimwa na bunge lenye wabunge wengi wa chama anachoongoza.

Katika uchaguzi wa chama, alikuwa anakabiliwa na upinzani kutoka kwa aliyekuwa waziri wake wa afya Zweli Mkhize, ambaye vile vile alitimuliwa kutoka baraza la mawaziri kutokana na sakata ufisadi, na wote wamekana kabisa madai yanayowaandaman.

Kuchaguliwa kwa Ramaphosa ni tabasamu ya muda kwake na wafuasi wake, kwa sababu bado anachunguzwa na polisi, ofisi ya ushuru na benki kuu kuhusiana na madai ya utakatishaji wa pesa, baada ya kuibwa kwa dola 580,000 zilizokuwa zimefichwa kwa kiti shambani mwake, na akakosa kuripoti wizi huo kwa mamlaka husika.

Kamati ya wataalam wa sheria iliyoteuliwa na spika wa bunge, ilisema katika ripoti yake kwamba Ramaphosa ana kesi ya kujibu, na kwamba huenda alivunja sheria za kupambana na ufisadi na katiba. Lakini bunge lilitupilia mbali ripoti hiyo na kumsafisha Ramaphosa. Amekanusha kabisa kufanya kosa lolote.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2024

Ramaphosa amepata ushindi mkubwa kuongoza chama cha ANC ikilinganishwa na ushindi aliopata mwaka 2017.

Ushindi huo unamueka katika nafasi nzuri ya kugombea mhula wa pili wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Viongozi wa Afrika kusini wamekuwa wakiondoka madarakani kutokana na Sakata za ufisadi, tangu alipoondoka Nelson Mandela.

Thabo Mbaki aliondoka madarakani akihusishwa na Sakata ya ufisadi, ya kujaribu kumficha Jacob Zuma wakati huo akiwa waziri.

Ngalama Mbontelthe naye aliondoka akihusishwa na Sakata ya ufisadi wad ola milioni 13.

Jacob Zuma alilazimika kuondoka kutokana na Sakata ya ufisadi ya ununuzi wa silaha uliopelekea Afrika kusini kupoteza mabilioni ya dola.

Aliyekuwa rais wa Afrika kusini Nelson Mandela alipokuwa katika gereza la Robben. Marais wote wa Afrika kusini walioingia madarakani baada ya Mandela wamehusishwa na kashfa za ufisadi.

Watu kadhaa katika ANC wanaandamwa na madai ya ufisadi

Mkhize naye anayetaka kumuondoa Ramaphosa katika chama cha ANC, alijiuzulu kutokana na kashfa ya ufusadi kuhusiana na pesa za kupambana na corona.

Chama cha ANC kimekuwa madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa mzungu mwaka 1994 na kina matumaini kuendelea kutawala nchi hiyo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Ukusanyaji wa maoni hata hivyo unaonyesha kwamba umaarufu wa ANC umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na Sakata hizi za ufisadi, ukosefu wa ajira na huduma mbovu kwa raia wa Afrika kusini.

Paul Mashatile amechaguliwa kuwa naibu wa kiongozi wa chama cha ANC. Anakuwa katika nafasi ya mbele kuchukua uongozi wa endapo Ramaphosa atalazimika kung’atuka kama joto la kisiasa litamzidi.

Watu wa karibu sana na Ramaphosa wameshita viti vingi katika uongozi wa chama hicho, ikiwemo katibu mkuu na mwenyekiti wa chama kitaifa.

Lakini hakuna mgombea yeyote kutoka mkoa wa Kwa Zulu Natal, ngome ya kisiasa ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, ameshinda nafasi yoyote ya uongozi wa juu wa chama.

Aliyekuwa mke wa Jacom Zuma, Nkosazana Dlamin Zuma, aliongoza wabunge waliopiga kura ya kutaka Zuma afunguliwe mashtaka.