Rais Zelensky anasema Ukraine inakabiliana vikali dhidi ya uvamizi wa Russia

Rais Volodymyr Zelenskey akitembelea wanajeshi wake kwenye handaki katika mstari wa mbele wa vita

Rais Volodymyr Zelensky anasema wa Ukraine wamefanikiwa kuzuia uvamizi wa Russia dhidi ya Kiyv na kuwataka wananchi kulilinda taifa lao.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amethibitisha Jumamosi kupitia ujumbe wa tweeter kwamba wanajesi wa nchi yake na wananchi wameweza kuzuia mpango wa uvamizi wa Russia kuuteka mji mkuu wa Kiyv, akitoa wito kwa wa-Ukraine kulinda taifa lao.

Katika siku ya tatu ya uvamizi wa Rashia dhidi ya Ukraine uloanzishwa na Rais Vladimir Putin zaidi ya raia 198 wa Ukraine wameuwawa na karbu 1, 115 wamejeruhiwa, kulingana na waziri wa afya wa ukraine Victor Liachko.

Milio ya bunduki imekua ikisikika katika mji wa Kiyv, kukiwa na ripoti za mapigano kati ya wanajeshi wa Russia kwenye vifaru na wanajeshi wa Ukraine katika mitaa ya mji huo.

Jeshi la Ukraine linasema shambulio la warashia kuteka kambi moja ya kijeshi lilirudishwa nyuma.

Afisa mmoja muandamizi wa wizara ya ulinzi Marekani akizungumza na waandihsi habari bila ya kutaja jina lake anasema, jeshi la Rashia limefyetua zaidi ya makombora 200 ikiwa ni pamoja na makombora ya aina ya Cruise tangu kuanza uvamizi ya kilenga vituo vya kijeshi.

Afisa huyo aliendelea kueleza kwamba wanajeshi wa Russia wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi na raia wa Ukraine na hata kurudishwa nyuma katika baadhi ya maeneo.

Afisa huyo amesema uwongozi wa kijeshi wa Ukraine uko thabiti.

Waziri wa mambo ya nchi za nje Antony Blinken ametangza kwamba Marekani inapeleka msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 350 kwa Ukraine ili kuisaidia serikali ya Kiyv kukabiliana na uvamizi wa Rashia.