Rais Xi wa China na Biden wa Marekani wanaweza kukutana katika APEC

Gavana wa California, Gavin Newsom, Jumatano alikutana na rais wa China, Xi Jinping, mjini Beijing, na kuzusha matumaini yake kwamba China, na Marekani, zitaafikiana katika masuala muhimu kabla ya mkutano wa APEC, jijini San Fransisco mwezi ujao.

Rais Xi, na mwenzake wa Marekani, Joe Biden, wanatarajia kukutana katika mkutano wa kiuchumi wa mataifa ya Asia na Pacific, APEC, huko San Franciso, Novemba 11 hadi 17.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili bado haujathibitishwa licha ya kwamba ziara iliyopangwa ya waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi, ya Washington leo hii pia inatazamiwa kufungua njia ya mkutano wa ngazi ya juu baina ya Marekani na China.

Rais Xi, katika taarifa kwa Newsom, kwa mujibu wa televisheni ya China, CCTV, imeeleza kwamba anatarajia ziara yake itawezesha maelewano ya pende zote na kuchukuwa jukumu muhimu katika kupanua ushirikiano baina ya China, na California, na kukuza uhusiano imara na wenye nia njema kwa China na Marekani.