Rais wa zamani wa Angola azikwa nyumbani

Rais wa zamani wa Angola na kiongozi wa chama tawala cha MPLA hayati Jose Eduardo dos Santos wakati wa uhai wake. Augosti 29, 2012. REUTERS/Siphiwe Sibeko.

Raia wa Angola na viongozi wa kigeni walikusanyika siku ya Jumapili kwa mazishi ya kiongozi wa muda mrefu Jose Eduardo dos Santos, ambaye alifariki nchini Uhispania mwezi Julai lakini mazishi yake yalicheleweshwa na ombi la familia ili kufanyika  uchunguzi wa mwili wake.

Mazishi ya Dos Santos, aliyefariki katika kliniki moja mjini Barcelona Julai 8 akiwa na umri wa miaka 79, yanafanyika siku chache baada ya uchaguzi kuonekana kukirejesha chama chake cha MPLA madarakani kutokana na matokeo ambayo yamepingwa na muungano mkuu wa upinzani nchini humo.

Dos Santos na familia yake walitawala siasa za Angola kwa miaka 38 aliyotawala, hadi mwaka 2017. Chama chake cha zamani cha Marxist, People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA), kilichokuwa madarakani kwa takriban miongo mitano, kinaonekana kimeshinda tena uchaguzi wa Jumatano.

Wakuu wa nchi na mawaziri wakuu kutoka kote barani humo, pamoja na rais wa Ureno, tawala wa zamani wa kikoloni nchini Angola, Marcelo Rebelo de Sousa.

Kuwepo kwa wageni kutoka nje ya nchi kumeiwezesha mamlaka kutaka kusitisha maandamano yanayoweza kutokea kuhusu kupingwa kwa matokeo ya muda ya uchaguzi yaliyotangazwa.