Rais wa zamani Carter atimiza miaka 100, wanahistoria watathmini mafanikio na kushindwa kwake

  • VOA News

Jimmy Carter thumbnail (AP)

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anatimiza miaka 100 huku waandishi na wanahistoria wakitathmini tena mafanikio yake na kushindwa na pia alikuwa  rais wa Marekani wa muhula mmoja tu.

Wakati aliporejea Plains, Georgia, mwaka 1981, rais wa zamani Mdemocrat Jimmy Carter alishindwa na kukataliwa na wapiga kura kwa ushindi mkubwa alioupata Mrepublican Ronald Reagan.

Mwandishi na mwanahistoria Jonathan Alter anasema “alipokuwa madarakani, alishindwa kisiasa. Lakini alikuwa na mafanikio makubwa na yenye mtizamo.”

Alter anatambua kile ambacho wengi wanakifahamu kuhusu Carter hivi leo –kazi ya hisani inayofanywa na Carter Center, “kupambania amani, kupigania maradhi, na kujenga matumaini,” kote duniani.

“Amefanya kazi nzuri sana ya kusimamia chaguzi katika zaidi ya nchi 100. Lakini marais wa zamani hawana mamlaka makubwa kama marais, na orodha ya mafanikio yake kama rais ilipuuzwa, haikuangaliwa kwa kina, au ilisahauliwa kabisa kwa muda mrefu sana,” anasema Alter.

Mzozo wa mateka nchini Iran, kupanda kwa mfumuko wa bei na marufuku ya mafuta katika miaka ya 1970, ilifanya muda wa Carter kuwepo White House, ugubike kazi yake.

Watu wakiandika kadi za pongezi kwa Jimmy Carter wakati wa kuadhimisha sikukuu yake ya kuzaliwa ya 99 kwenye kituo cha Carter Center, Atlanta, Sept. 30, 2023.

Hata hiyvo, wasifu wa Jimmy Carter “ His Very Best,” ulioandikwa na Alter ulikuwa miongoni mwa mambo ambayo yalijumuisha miaka yake minne katika White House ilikuwa na mambo mengine lakini siyo kushindwa.

Alter anasema “siyo tu mikataba ya Camp David na kufungua mahusiano na China, lakini mlolongo mrefu wa mafanikio ya kisheria kuhusu mazingira na masuala mengine mengine.”

Carter alitia saini sheria ya 1980 ya Alaska National Interest Lands Conservation kulinda zaidi ya hekta milioni 40.5, ambayo inaangaziwa kuwa moja ya sehemu muhimu sana ya sheria ya mazingira iliyowahi kupitishwa.

Joe Crespino wa Profesa historia katika Chuo Kikuu cha Emory anasema Carter mara kwa mara alikuwa akikutana na wanafunzi wake huko Atlanta kujadili maamuzi mazuri na mabaya aliyofanya wakati alipokuwa rais.

Crespino anasema “nadhani nitamkumbuka Rais Carter kama rais ambaye alihudumu katika kipindi kigumu sana, alilazimika kukabiliana na hali ambazo zilikuwa juu ya uwezo wake.” Na kuongezea “kuweka masuala ya haki za binadamu mbele na juu katika sera ya Mambo ya Nje ya Marekani. Hakuna rais aliyefanya hivyo kama alivyofanya Jimmy Carter. Ilikuwa ni muda muhimu sana katika kubadili uwiano wa madaraka katik enzi ya Vita Baridi.”

Crespino anasema baadhi ya mafanikio ya ndani ya nchi ya Carter hayakuangaizwa ikiwa ni pamoja na kuisuka tena serikali kuu na usimamizi wa mashirika ya ndege, magari makubwa na viwanda vya bia.

Andrew Young

Mmoja wa wajumbe wa baraza la mawaziri la Carter, alikuemo balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Andrew Young, ambaye anashukuru Carter kuishi kwa muda mrefu kushuhudia tafsiri ya urithi wake wa ukarimu. “Hakuna sehemu katika dunia ambayo naifahamu ambako watu hawana mambo mazuri ya kumzungumzia, iwe mafanikio au la,” ameongezea Young.

Dunia inaendelea kunufaika kutokana na kazi za kituo cha Carter kupambana na magonjwa kama Guinea worm, ambapo kesi za ugonjwa huo zimepungua barani Afrika na huenda ikawa ni janga la pili la ugonjwa kuwahi kutokomezwa.