Rais wa Yemen asema hataachia madaraka ikiwa mpinzani wake Jenerali aliyeasi jeshi atakuwa bado na ushawishi na nguvu.
Rais wa Yemen Ali Abdalla Saleh amesema hataachia madaraka ikiwa mpinzani wake mkuu , jenerali mkuu aliyeasi na kuhamia upinzani na kiongozi wa kikabila bilionea na familia yake watakuwa bado wana nguvu na ushawishi nchini humo.
Kaatika mahojiano maalum na Washington Post na jarida la Times , Bw. Saleh alisema mpango wa mpito wa kisiasa uliopangwa na majirani wa Yemen kwamba vigezo vyote vinavyochangia ghasia za kiraia nchini humo lazima viondolewe.
Hiyo inamaanisha hataachia madaraka kama Jenerali Ali Mohsen al Ahmar na Hamid al Ahmar, mfanyabiashara tajiri wa mawasiliano na mwanasiasa ambaye kaka yake anaongoza kabila lenya nguvu kuliko yote Yemen wanaruhuisiwa kugombea katika uchaguzi ujao.