Rais wa Vietnam awasili Tanzania kwa ziara rasmi

Rais wa Vietnam,Truong Tan Sang, amewasili Tanzania kwa ziara ya siku tatu.

Watanzania wametakiwa kutumia fursa ya ujio wa Rais wa Vietman, Troung Tang Sang pamoja na wafanyabiashara wa nchi hiyo kutafuta mbinu ya kutumia raslimali zilizopo nchini Tanzania kupata maendeleo ya kiuchumi.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Dina Chahali wa Dar es Salaam, Tanzania

Rais wa vietnam Trough Tang Sang pamoja na ujumbe wake wapo nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na Vietnam.

Rais huyo wa Vietman alipokewa rasmi ikulu jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano na mwenyeji wake Rais wa Tanzanai John Magufuli ambaye alisisitiza rai hiyo kwa watanzania kutumia fursa ya ziara ya ujumbe wa Vietman kuinua uchumi wa Tanzania ambao mpaka sasa bado ni miongoni mwa nchi maskini duniani.

Kiongozi huyo wa Vietman aliambatana na ujumbe wa watu 51 ambao ni wafanyabishara pamoja na baadhi ya mawaziri kwenye serikali yake.

Rais wa Tanzania, John Magufuli



Rais wa Tanzania, John Magufuli na mwenzake wa Vietnam walifanya mazungumzo maalum Ikulu jijini Dar es Salaam yaliyojikita katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ikiwemo kupanua wigo wa uwekezaji utakaochochea biashara kati ya Tanzania na Vietnam pamoja na kukubaliana kuwekeana mikataba ya kutowatoza kodi mara mbili wawekezaji na wafanyabishara wanaowekeza katika nchi hizi.

Bwana Sang pia atashiriki mkutano wa biashara na uwekezaji unaotarajiwa kuhudhuriwa na taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
--------------------------------------------------------------------------------------------------