Rais wa Ukraine, atetea msaada wa Marekani

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, Jumatano ametetea uamuzi wa utawala wa rais wa Marekani, Joe Biden, wa kuipa Kyiv, mabomu ya rashasha, silaha zilizopigwa marufuku na zaidi ya nchi 120 kwa uwezo wake wa kuua kiholela.

Amesema silaha hizo zitaisaidia Ukraine, kujilinda kutokana na uvamizi wa Russia.

“Ni rahisi sana kukosoa mabomu ya aina hii,” rais Zelenskyy alisema kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na Rais wa Marekani Joe Biden.

“Uamuzi huu utatusaidia kutuokoa,” aliongeza kusema.

Uamuzi wa Washington umezua mjadala miongoni mwa baadhi ya washirika wa NATO, ambao wengi wao ni walitia saini mkataba wa kupiga marufuku silaha za aina hiyo.

Kiongozi huyo wa Ukraine alibainisha kuwa Moscow inatumia mabomu ya hayo katika uwanja wa vita.

Amesema “sikusikia baadhi yenu nchi zikiikosoa Russia,” kwa hili.