Akiwa nchini humo Rais Macron anatarajiwa kutembelea eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbari nje kidogo ya mji mkuu Kigali. Na baadaye atafanya mkutano na waandishi akiwa na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda kabla ya kufungua rasmi jumba la utamaduni wa Ufaransa mjini Kigali
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa Alhamis kuanza ziara ya siku mbili nchini Rwanda ziara ambayo inatajwa kama ya kihistoria ili kujaribu kufufua uhusiano wa nchi hizo mbili ulioharibika zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Hali ya sintofahamu baina ya nchi hizi mbili ilianza baada ya kumalizika mauaji ya kimbari mwaka 1994 dhidi ya jamii ya watutsi wa Rwanda ambapo Rwanda inaishutumu Ufaransa kuisaidia serikali ya hayati Rais Juvenali Habyarimana, Rais wa zamani wa Rwanda ambaye serikali yake inatajwa kuandaa na kutekeleza mauaji hayo.
Your browser doesn’t support HTML5