Rais wa Somalia kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Uturuki

  • VOA News

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud. Picha ya maktaba.

Maafisa wa Somali wamesema Jumanne kwamba Rais wao Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, wamepanga kukutana ana kwa ana mjini Ankara, Uturuki.

Vyanzo vya karibu na ofisi ya Urais wa Somalia vimeithibitishia VOA kuhusu mazungumzo hayo, kuwa Ethiopia aliitisha mkutano huo naye Rais wa Somalia akaubali.

Vyanzo hivyo viliongea katika misingi ya kutotajwa kwasababu hawakuidhinishwa kuongea na vyombo vya hsbsri kwamba mkutano huo unatarajiwa kufanyika Jumatano. Wameongezea kuwa rais wa Somalia aliwasili Uturuki kwa mwaliko wa Rais Tayyip Edorgan.

Maafisa wa Ethiopia hata hivyo hawajathibitisha kuhusu mkutano huo. Iwapo utafanyika, basi utakuwa wa kwanza kati ya viongozi hao, tangu Ethiopia na Somalia kugubikwa na mzozo wa mkataba wa bahari, ambao Ethiopia ilitia saini na jamhuri iliyojitenga ya Somaliland hapo Januari mosi.

Mkataba huo unaipa Ethiopia fursa ya kilometa 20 za mwambao wa Bahari ya Sham karibu ya Ghuba ya Aden, kwa makubaliano ya kutambua uhuru wa Somaliland. Ethiopia inasisitiza kuwa haijakiuka uhuru wa Somalia.