Wengi wanawaza kuhusu vita vinavyoendelea kwa jirani wa Poland, Ukraine na matarajio kwamba kurejea tena kwa Donald Trump kwenye Ikulu ya Marekani kutaleta mabadiliko ya kiusalama kwenye eneo hilo.
Baadhi pia wanaogopa kuwa huenda Trump akaondoa Marekani kwenye NATO, au afanye mkataba na rais wa Russia Vladimir Putin, ambao utahalalisha maeneo ya Ukraine yaliyochukuliwa na Russia, huku Russia ikipata ari ya kivamia mataifa mengine pia.
Baadhi pia wanaamini kuwa Trump ataweza kushawishi Putin kusitisha mapigano hayo. Duda ambaye ana urafiki wa karibu na Trump wakati wa hotuba yake mjini Warsaw amesema kuwa Ulaya itaendelea kuhitaji ulinzi wa Marekani.
Amesema kuwa hakikisho la ulinzi kutoka kwa marais tofauti wa Marekani, ni muhimu sana kwenye nyakati hizi za uchokozi mpya kutoka Russia.