Rais wa Palestina Mahamoud Abbas Alhamisi alitoa wito kwa jumuia ya kimataifa, hasa Marekani, kuacha kuipa silaha Israel ili kukomesha umwagikaji wa damu katika Ukingo wa Magharibi na huko Gaza.
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Abbas ameitaja Marekani kwa sababu ya shehena zake za silaha na kura zake za turufu katika maazimio ya Baraza la usalama kwa kulaani vita vya karibu mwaka mmoja kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas huko Gaza.
“Sitisha uhalifu huu. Usitishe mara moja. Acha kuuwa watoto na wanawake. Sitisha mauaji ya kimbari. Sitisha kutuma silaha kwa Israel,” Abbas alisema.
“Huu wendawazimu haupaswi kuendelea. Dunia nzima inawajibika kwa yale yanayotendewa watu wetu huko Gaza na Ukingo wa Magharibi,” aliongeza.