Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi, amedaiwa kuhusika na kushindikana kwa miradi mikuu unaohusika na kashfa ya “Tuna,” amesema mmiliki kampuni ya Emarati na Lebanon ya utengenezaji meli ya Privinvest, katika mahakama kuu ya Uingereza, Jumatano.
Kampuni ya Privinvest, na mmiliki wake kutoka Ufaransa, Iskandar Safa, wanakabiliwa na kesi ya dola bilioni 3.1 kutoka taifa hilo la Afrika kwa shutuma za kulipa mamilioni ya dola za rushwa kwa maafisa wa Msumbiji, na benki za Credit Suisse.
Msumbiji inadai zaidi ya dola milioni 136 zililipwa ili kupata upendeleo wa kufanya miradi mitatu kati ya mwaka 2013 na 2014, ikijumuisha mmoja kutumia vibaya ukanda wa bahari wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa samaki aina ya jodari.
Kampuni ya Privinvest na Safa zimepinga kushiriki matendo yoyote mabaya, na kusema malipo yoyoye yalifanywa kinyume cha sheria.
Wamesema kesi hiyo ina maslahi ya kisiasa ili kuepusha lawama dhidi ya rais Nyusi na maafisa wengine waandamizi.