Rais wa Nigeria apendekeza mabadilko ya katiba

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Rais wa Nigeria GoodLuck Jomathan katika juhudi za kufanya mabadilko ya katiba ataka wanasiasa wafanye kazi kwa muhula mmoja.

Rais wa Nigeria anapendekeza marekebisho ya katiba ili kuweka muda maalum kwa marais na magavana kufanya kazi kwa muhula mmoja ambao ni mrefu zaidi.

Rais Goodluck Jonathan alitangaza mpango wake jana jumanne akisema anategemea itawaruhusu wanasiasa kupunguza kufikiria kuchaguliwa tena . Rais huyo pia alisema pia itasaidia kuokoa fedha kufanya uchaguzi mara chache zaidi.

Maelezo yake hayakueleza muhula utakuwa ni wa muda gani , katika sheria iliyopo kila muhula una miaka minne na kuna kikomo cha mihula miwili.